YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 16 OF 31

Taifa la Israeli walikuwa mzabibu wa Mungu, lakini wakageuka wakawa mzabibu mwitu usiofaa. Nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?(Yer 2:21). Sasa Yesu anajitangaza kwamba yeye ndiye Mzabibu wa kweli. Matawi ni wale wakaao ndani yake (m.5). Wakaao ndani yake ni hao ambao neno lake hukaa ndani yao (m.3 na 7). Je, wewe ni mmoja wao? Tambua kwamba Yesu siye shina tu, bali ni mzabibu wote, yaani shina pamoja na matawi! Hii inaonyesha umoja mkubwa ulioko kati ya Yesu na walio wake (m.5)! Yeyeanatufanya tuzae matunda mema!

Scripture