YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 17 OF 31

Zaburi ya 120 hadi ziliimbwa na waabudu walipokuwa safarini kwenda Yerusalemu wakati wa sikukuu. Zaburi hii inaadhimisha ulinzi wa Mungu katika maisha mazima. Msafiri anapitia nchi yenye milima akikumbuka kwamba Mungu aliyeumba milima yote atamhifadhi na kumsaidia daima. Hata usiku akilala kando ya njia, Mungu, ambaye kamwe halali usingizi, hukesha juu yake. Mungu atamlinda katika hatari zote usiku na mchana. Katika safari yake atamleta Yerusalemu salama na hata kumrudisha nyumbani kwake tena.