YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 13 OF 31

Mambo mawili ni wazi: 1.Kwa kila anayemwamini Yesu kumeandaliwa mahali kwa Mungu Baba Mbinguni (m.2-3)! Yesu anasisitiza: mnamakao mengi. Yaani, usiwe na mashaka! Ameshaandaa mahali kipekee kwa ajili yako. Ni kama ilivyo hapa duniani unapoalikwa kwenye sherehe. 2.Njia ya kufika Mbinguni ni mojatu (m.6)! Mtu asipokubali kumkiri Yesu Kristo alivyoshuhudiwa katika Biblia, hawezi kuingia uzimani. Mimi ndimi njia ... mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi(m.6; ling. Mdo 4:12:Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo)!

Scripture