YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 12 OF 31

Kutoka kwa Yuda kunamfanya Yesu aseme: Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake(m.31). Kwa nini? Kwa sababu kukamatwa kwa Yesu kumekaribia sana kutokana na kazi ya Yuda kumsaliti. Na njia ya Yesu kutukuzwa ni kifo cha msalaba. Yesu amenawisha miguu ya wanafunzi wake, na sasa atakwenda kutoa uhai wake kwa ajili yao. Na hutaka wafuate mfano wake: Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi (m.34; ling. 1 Yoh 3:16-18: Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli)!

Scripture