Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Kifo cha mfalme Sulemani kilisababisha taifa la Israeli kugawanyika katika Kaskazini (Samaria) na Kusini (Yerusalemu). Watawala wa Kaskazini waliabudu sanamu. Hivyo wakawafanya watu wasiende Yerusalemu kumwabudu Mungu. raia waliongozwa wamwasi Mungu. Nabii anawaonya watu wa upande wa Kusini (Yuda). Anawataka watubu kabla hawajaadhibiwa kama itakavyokuwa kwa wenzao wa Kaskazini. Wewe unaitwa kumwabudu Mungu ambaye amejifunua katika Kristo. Ukiwa kiongozi usiwapotoshe watu hata wamwasi Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

