Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Mungu ni mtakatifu na anaelewa yote tofauti na wanadamu walivyo. Mungu anaielewa hali yetu dhaifu. Mwokozi wetu anajishughulisha na kila mmoja wetu kwa jinsi alivyo. Kwa nini anafanya hivyo? Ni kwa vile ametuumba, ametukomboa, ametutakasa na hututunza kwa uweza wake. Mungu ametupa wajibu wa kuwatunza wengine kama tutunzwavyo sisi. Watu wana mahitaji tofauti. Kila mmoja umtendee kadiri ya anavyohitaji bila kuuharibu utu wala roho yake. Uwatendee wanaokuzunguka kama Mungu akutendeavyo wewe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

