Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Ni Mungu tu anayeweza kuuondoa uovu na mazao yake ambayo ni dhambi. Kum 28:49-52 na 64 inasema hivi:Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake; taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza.Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako.... Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. Hali ya kiroho ya taifa la Mungu inalinganishwa na miiba mikavu inayovunjwa na kuchomwa moto. Katika Biblia miti huwakilisha maisha ya kiroho. Matawi ni alama ya watu wamtumikiao Mungu. Majani ya miti hupukutika na kudondoka chini. Taifa linaweza kunyauka kutokana na uovu wake, na likakosa maana. Wewe ni tawi la aina gani? Je, hali yako ya kiroho imepukutika? Tafakari kuona kama uko imara katika eneo hili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

