Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Leo ni mwanzo wa majira ya Majilio, kipindi cha kujiandaa kwa ujio wa Yesu Kristo. Ni kipindi cha faraja, maana tunaambiwa Mungu amewakumbuka waliochoka katika mateso na vifungo. Ujio wa Yesu ni uhuru kwao waliofungwa na kukaa katika hali ya maombolezo. Yesu anasem:Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
  Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa(m.18-19). Furaha ya kweli na uhuru wa nafsi tutavipokea Yesu akiingia mioyoni mwetu. Je, katika majira haya ya majilio umekusudia kufanya nini? Kumbuka maandalio ni muhimu. Tumkaribishe Yesu ayatawale maisha yetu, kwani yeye ni Mfalme wa Amani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

