Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 13 YA 30

Taabu na mahangaiko yaletwayo na maadui wa Mungu havina nafasi ya kuwatesa watu kila siku. Kuna wakati wa mageuzi. Mapinduzi haya yatawagusa watu wote. Wasioona na wasiosikia watapewa kuona na kusikia. Wanyenyekevu watapata kicheko. Kuna shangilio la ushindi uletwao na Mungu Mtakatifu. Wasababishao adha watakomeshwa. Ni wakati wa wokovu na utawala wa Mungu. Mabadiliko yanaletwa na Kristo. Uvunjifu wa haki na amani vinakoma. Ulimwengu utajaa furaha, ufahamu, haki na hali ya kumsifu Mungu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz