Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 14 YA 30

Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana Bwana amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi(Isa 1:2).Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso(Zab 46:1). Israeli ilipaswa kumtegemea Mungu katika hali zote. Kinyume na hivyo ni kuasi. Aghalabu watu hupindisha mipango ya Mungu. Walipokuwa hatarini waliasisi uhusiano wa ulinzi na nchi jirani. Huko ni kumwacha Mungu. Ndiko kutafuta jibu rahisi kwa mambo magumu. Hata uwapo shidani, wasiliana na Mungu. Jina la Rahabu hapa linawakilisha Misri, iliyopoteza nguvu. Ni mfano wa sanamu ya mtu iliyowekwa shambani kutisha ndege. Taifa linapaswa lisitegemee taifa jingine zaidi ya Mungu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz