Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Ufalme wa Kusini uliitwa Yuda. Jina la Israeli lilitumika kwa ufalme wa Kaskazini pekee. Kwa sababu ya hofu ya kuvamiwa na Wasiria, Yuda ilifanya mapatano na mataifa ya jirani ili kupata msaada wa kiulinzi. [Mfalme wa Ashuru] alisikia habari ya Tirhaka, mfalme wa Kushi, ya kwamba, Ametoka ili kupigana nawe; naye aliposikia hayo, akatuma wajumbe kwa Hezekia, kusema,Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.Tazama, umesikia habari ya mambo yote, ambayo wafalme wa Ashuru wamezitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa je! Utaokoka wewe? (Isa 37:9-11). Mungu anawakemea kwa kufanya agano la kifo. Anasema atafuta mpango huu wa uovu wa usalama wa muda tu. Ili kupata usalama wenye uhakika, umtazame na kumtegemea Mungu. Msingi wa mtu wa Mungu ni Kristo. Maisha yako yote yashikamane naye. Unabii kuhusu Kristo unasema hivi:Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni(Zab 118:22).Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo(1 Pet 2:6-8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

