Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 12 YA 30

Arielini jina la Yerusalemu ambapo madhabahu ya Mungu ipo. Ni jina la mfano. Isaya anakemea hali ya unafiki wa kidini. Uhusiano wa mtu na Mungu haulingani na ule wa wafanyabiashara. Maisha ya kiroho si kutimiza desturi maalumu za ibada kama kufunga na kutoa sadaka. Ibada ya kweli ni kuhusiana na Mungu. Matokeo yake ni kutenda haki na kuhurumia watu.Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja?Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza(Mik 6:6-9).Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na uudi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii(Yer 6:20). Moyo ni kiini cha maisha ya kiroho. Nia ya moyo ndiyo impendezayo Mungu. Yesuakawaambia [Mafarisayo], Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu(Mk 7:6-9).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz