Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Pamekuwa na vilio katika nchi nyingi kote duniani, katika masuala ya kutotenda haki na kupenda rushwa katika tawala zao. Mtunga zaburi hii anashughulika na watu wanaosababisha hayo kutokea. Yaani katika vyombo vya kutolea haki na maamuzi kama vile mahakama na vinginevyo, walio haribika kwa kupokea rushwa. Uovu wa mawazo na vitendo vyao, wala kutosikia kabisa vilio vya watafuta haki. Lakini Mungu hupendezwa na wale wenye kupenda na kutenda haki. “Hakika iko thawabu yake mwenye haki” (m. 11b).
Angalia, nukuu hii, pamoja na nukuu nyingine zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

