Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 7 YA 30

Yatupasa kutambua kwamba kuwa mbali na Mungu kunaanzisha maumivu makali. Kubaki katika hayo kunaongeza uchungu. Lakini tunapomrudia Mungu kwa maombi na toba, tunaahidiwa kwamba tutahuishwa tena. Wengine wengi wakimwacha Mungu na kukudharau, wewe usiwafuate. Endelea kumwomba Mwokozi wako. Hata kama unakabiliwa na mambo magumu kila upande wa maisha yako, usikate tamaa. Lipo tumaini pale unapoamua kumtegemea Mungu. Je, uko tayari kumngojea Mungu kwa uvumilivu hadi atakapotenda kwa ajili yako?

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz