Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Fungu hili ni zaburi iliyojaa imani, sifa na tafakari kumhusu Mungu na ukuu wake. Wanaomtegemea Yesu wataimba wimbo wa sifa, kwa sababu yeye ataasisi wokovu na kutawala milele. Duniani kuna shida zinazotuzonga. Lakini Mungu ametuhakikishia kutupa amani hata katika taabu. Vurugu zilizopo haziwezi kututikisa, kwa kuwa tunalo pendo na uweza wa Mungu visivyobadilika. Kwa hiyo,msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu(Flp 4:6-7). Unatafuta amani? Mtazame na umtegemee Mungu pasipo kukata tamaa wala kuchoka. Tafakari m.8-9, na uitumie kuwa sala yako leo:Katika njia ya hukumu zako sisi tumekungoja, Ee Bwana; shauku ya nafsi zetu inaelekea jina lako na ukumbusho wako. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; maana kuhumu zako zikiwapo duniani, watu wakaao duniani hujifunza haki.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

