Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Mungu alilionya taifa la Yuda kuwa lisifuate msaada na usalama wa kijeshi kutoka Misri na kwingine. Nguvu za kijeshi hazina uwezo wa kuokoa. Ni Mungu pekee aletaye ukombozi. Taifa na watu wake wasubiri na wategemee uweza wa Mungu. Mamlaka ya Mungu hayasukumwi na watu. Hatuwezi kufanya lolote kwa Mungu ila kushukuru tu. Wokovu wa kweli unatoka kwake. Kwa kuwa tumeokolewa, tuishi kwa imani tukiamini kuwa atatupa nguvu ya kuyakabili matatizo. Tumsubiri Mungu, atatenda kwa wakati wake.Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba(2 Pet 3:9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

