Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 3 YA 30

Kwa kuwa Mungu ni mwumbaji anayo mamlaka juu ya kila kitu. Si nia yake kuiteketeza kazi yake. Bali uovu utendwao na watu wasiomtii Mungu unaleta hasira ya Mungu dhidi ya uumbaji wake. Ipo siku ambayo Mungu atauhukumu uumbaji wake. Dhambi inayofanywa na watu inaathiri viumbe vingine. Ukame, njaa, uhalifu, uharibifu wa mazingira na umaskini vinaletwa na uovu wetu. Dhambi inaharibu mfumo wa maisha. Pia watu waaminifu kwa Mungu wanateswa kwa sababu ya uovu uliopo. Mtu wa Mungu, endelea kuukataa uovu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz