Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Hukumu ya Mungu inalenga kuwafanya watu kuwa waaminifu kwa neno lake na kuimba kwa ajili ya utukufu na haki yake. Utukufu na haki ndiyo utakatifu wa Bwana. Hali mbaya ya wakati wa Isaya ilimfanya alie na kuomboleza. Sisi pia tunaweza kuwa tunanyong’onyezwa na hali ya uovu na dhambi zilizopo na zinazofanywa leo. Hata tuwapo katika hali hiyo, tunatakiwa kutegemea ahadi ya Mungu na kusonga mbele tukitazamia kuimba nyimbo za sifa kwa ajili yake. Hakika Mungu anakusudia kuziokoa mbingu na nchi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

