Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Watakatifu ni akina nani hasa? Ni wale wamwaminio Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Baadhi yao wako hai:Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao(Zab 16:3) Na baadhi yao walikufa katika imani hiyo:Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza(1 The 4:16). Kanisa linaadhimisha sikukuu hii kuonyesha kuwa wapo mashahidi wa Kristo waliodumu katika imani hadi kufa, na kwamba siku ya mwisho wataonekana mbele za uso wa Kristo kama washindi.Tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awazaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mawazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao(m.9). Tunatamani kuwa sehemu ya kundi hili la watakatifu. Basi tuishi kwa utii wa imani, ili Yesu akija, atukute tuko safi kiroho.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

