Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Katika Isa 9-11 tumeona Mungu awezavyo kuwaadhibu watu. Wimbo huu wa sifa huonesha lengo la Mungu na matokeo yake kwao waliomkimbilia katika hali hiyo ngumu. Wanamshukuru Mungu hata kwa hasira yake, kwa kuwa kupitia hiyo walijifunza kuwa yeye ndiye wokovu wao. Basi, tuteke maji ya uzima katika visima vya wokovu, ili na sisi tuwe watu wa shukrani daima, watu tunaofarijiana katika Kristo na kushuhudia kwa wote juu ya ukuu wa upendo wa Mungu na ukombozi aliotukirimia bure kwa njia ya kifo chake Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz