Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 24 YA 28

Mungu alitumia Waashuru kuadhibu Israeli, lakini hili halimpi mfalme wao sababu ya kujisifu. Mungu atamwadhibu kwa sababu ya majivuno yake. Je, mwisho wake ni maangamizo katika nchi yote? Hapana! Hata katika hukumu hizo Mungu anahakikisha kwamba kuna “mabaki”, yaani watu waliopona. Kuhusu hao imeandikwa kwambaMabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga(= Mfalme wa Ashuru), bali watamtegemea Bwana, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli(m.20). Mungu anaweza kuadhibu na kuondoa ulinzi juu yetu ili tusiwategemee watu wala mafanikio yetu, bali tufikie kumkumbuka Mungu na kumtegemea yeye kwa kweli. Hebu tujifunze kumshukuru na kumsifu Mungu kwa ajili ya hiyo.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz