Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Unabii unaonesha kuwa atapatikana Masihi kutoka ukoo wa Daudi. Huyu atakuwa mfalme wa haki na amani, na utawala wake utadumu milele. Nia yake ni kuwatoa watu kutoka kwenye maisha ya giza na kuwaingiza kwenye maisha ya nuru. Tunaona kwamba jambo hili limekuwa na mwendelezo hadi wakati wa kuzaliwa kwa Yesu, tukilinganisha m.1-2 na Mt 4:12-16:Yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa. Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza(m.1-2).Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia (Mt 4:12-16). Unabii huu unatuhusu sana sisi wa kizazi cha leo, maana kwa kuzaliwa kwa Yesu nuru imeletwa kwetu. Hivyo maisha ya giza yasiwe na nafasi kabisa kwetu tunapomfuata Yesu kwa imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz