Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Mungu alitumia Ashuru kuwapiga Waisraeli kwa fimbo wasibaki katika kujivunia. Katika mazingira haya hata “watu wakaao katika Sayuni” (neno la mfano kwa wamchao Mungu) wanaweza kuogopa Ashuru na kukata tamaa. Somo la leo linatujia ili kuleta sura mpya kwamba Mungu ameona na anasema tusiogope:Msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri(m.24). Mungu ataingilia kati na kuwashindia watu wake. Hivyoitakuwa katika siku hiyo mzigo wake(= Mfalme wa Ashuru)utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta(m.27). Basi tusiache kumlilia na kumweleza machungu yetu, bali tufanye ilivyoandikwa katika m.30:Piga kelelesana, Ee binti Galimu; sikiliza, Ee Laisha; ole wako, maskini Anathothi!Mungu atatujibu kwa wakati wake. Tuviinue vichwa vyetu na kumtazamaAliye mwenye uweza(m.33)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz