Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 26 YA 28

Huu ni wimbo kumhusu mkombozi ambaye ana sifa, vipawa, karama na nguvu za Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni mkombozi ambaye anaasilika na ukoo wa Daudi. Anakuja akiwa na roho ya unabii, utawala wa haki, na utakatifu. Atarudisha furaha, amani na umoja (rudia mwenyewe m.6-9). Soma kwa makini mistari ifuatayo:Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake(Mt 3:16). Yohana aliyembatiza Yesu anashuhudia:Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake(Yn 1:32). Na baada ya Yesu kupaa mbinguni, Petro anahubiri:Mungu alimtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye(Mdo 10:38). Bila shaka picha tunayopata tunaposoma mistari hii ni kwamba mkombozi huyu ni Kristo Yesu. Amekuja kufundisha, kutangaza amani na kuponya, na kutufungua kutoka minyororo ya dhambi. Wajibu wetu ni kukubali akomboe maisha yetu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz