Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Mungu hasahau watu wake. Hata kama watatawanyika na kuishi uhamishoni, atawakumbuka, na siku moja atawakusanya tena.Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia(m.11-12). Ninyi mlio watu wa Mungu, ujumbe huu ututie moyo ambao tunaendelea kumwamini. Hata kama maisha yetu leo yanaonekana hayafanikiwi sana, hii haimaanishi kuwa Bwana ametusahau. Jicho lake linatuona, na mkono wake unatuchunga. Yesu atakapokuja kulichukua kanisa lake, ndipo itadhihirika kuwa alikuwa bado anatutambua na kutukumbuka. Tusirudi nyuma katika imani, tuendelee kumwabudu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz