Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 23 YA 28

Yaliyotokea wakati wa Isaya, yapo hata sasa. Kuna baadhi ya mila zinazowanyang’anya wajane na yatima haki zao. Kwa mfano baba mwenye familia akifa, baadhi ya taratibu za makabila fulani zinamlazimisha mjane kurithiwa au kuondoka kwenye nyumba aliyoishi na mume wake, kisha ndugu wa marehemu hugawana mali zote na kuwaacha yatima na mjane mikono mitupu. Hapa tujiulize kanisa liko wapi kuwatetea wahanga hawa? Neno lituonye dhidi ya uonevu huo na kutusukuma kuwatetea wajane na yatima.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz