Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Siku zote duniani kuna watu wanaomsikiliza na kumtii Mungu na wengine ambao hawataki kumsikiliza wala kumtii. Wacha Mungu wasikatishwe tamaa na maneno ya wale wasiomtii Mungu, wala wasionee wivu kile kinachoonekana kama mafanikio ya wanaomtii. Badala yakewaende kwa sheria na ushuhuda(m.20a). Maana yake, tubaki katika imani! Bwana akiwa hofu yetu, atakuwa mahali patakatifu penye ulinzi kwetu, wakati atakuwa jiwe la kujikwaza kwa wasiomtii. Mafanikio yao hayatadumu, hawawezi kwenda nayo mbinguni, ila utakatifu wa mcha Mungu ndio unaotupeleka mbinguni.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz