Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 22 YA 28

Watu wa Israeli (= Ufalme wa Kaskazini) wanalaumiwa kwa kuwa na jeuri, kuasi, kutotenda haki, na kuwa wanyanyasaji. Hata walipoadhibiwa hawakugeuka. Walikataa kutambua kuwa Mungu ndiye aliyewaadhibu vikali namna hiyo, naye ataendelea wasipotubu. Watakuwa naWaashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. ... Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. ...Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa(9:12, 17, 21). Tukio hili litufundishe kuwa ikiwa sisi tumemkosea Mungu na akatuondolea amani, kama tusipogeuka na kutubu, hakika tutaadhibiwa. Kwa hiyo kila mmoja atafakari ni wapi alipomkosea Mungu, kisha ageuke na kutubu. Uponyaji upo pa Mungu tu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz