Siku 21 za KufurikaMfano

Kuongeza Upendo Wangu kwa Mungu
Katika Luka 10:25-37, Yesu anatatua mambo mawili. Siyo tu analinganisha kila amri na unabii katika mambo mawili, Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako, lakini pia anafungamanisha upendo kwa Mungu na upendo kwa watu pamoja. Yesu anamueleza muuliza swali kile ambacho Biblia imetuelekeza wote siku zote: kadri tunavyompenda Mungu, ndivyo tutakavyowapenda watu. Kwa kadri tutakavyowahurumia watu, ndivyo tunavyoonesha ni kiasi gani tunampenda Mungu. Hatuwezi kujawa na Roho Mtakatifu na kushindwa kutembea katika upendo.
Kama tukiwachukia watu kwa sababu ya rangi yao, ukabila wao, walichotufanyia, au walichosema juu yetu, Biblia inasema sisi ni kama wauaji. Tunajua wauaji hawana sehemu katika ufalme wa Mungu. Kama tukitembea katika Roho, lazima tutembee katika upendo. Kumbuka, amri zote zimefungwa katika upendo.
Hebu tuangalie tena katika 1 Yohana 2:15-17, tuliyosoma hapo awali katika mpango huu. Inazungumza juu ya wale wanaompenda Mungu na wale wanaoupenda ulimwengu huu. Angalia kuna makundi mawili tofauti. Na kifungu kinaainisha wazi kwamba wale wanaoshikilia upendo wa ulimwengu na anasa zake hawana upendo wa Baba ndani yao.
Mwishoni, Yohana 14:21 imeandikwa kutuelekeza jinsi ya kuuonesha upendo wa Mungu kwa Mungu – kwa kuzishika amri zake. Tunapozishika amri zake, tunamuonesha kwamba tunamheshimu, tunamwabudu, na mwishowe tunampenda.
Wakati kuabudu ni muhimu, kumpenda Mungu ni zaidi ya kuliabudu jina lake jumapili asubuhi. Lazima tufuate amri zake, lazima tupende vitu anavyovipenda, na lazima tuoneshe upendo kati yetu.
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More