Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 10 YA 21

Kuachana na Ufujaji wa Maisha

Tunashauriwa kuishi maisha yetu kwa uangalifu na si kwa ufujaji. Ufujaji wa maisha ni maisha tunayoishi kujitukuza wenyewe, mapenzi yetu, na agenda zetu pasipokujali kusudi la Mungu. Maisha ya uangalifu ni maisha unayoishi kumtukuza Mungu, kuwa vile anavyopenda, kufanya mapenzi yake, na kuhakikisha kusudi lake linatimia katika maisha yetu.

Tunapokuwa tumejawa na Roho, maisha yetu yanakuwa dhahiri tofauti kwa yeyote anayetuona. Tunapokuwa hatufanyi kazi katika hekima za mwanadamu, na ufujaji wa tabia za mwanadamu, ni dhahiri kwa wote kwamba tunafanya kazi katika njia ambayo ni tofauti na watu wengine wote.

Waefeso 5:5-18 inatupa mengi ya kufikiria. Inazungumza kinyume sana kuhusu "matendo ya giza yasiyozaa" na badala yake inatushauri kutafuta kile kinachompendeza Bwana na kukifuata. Unadhani nini kinampendeza Bwana katika maisha yako? Unakifuata kwa moyo wote?

1 Yohana 2:16 inaendelea kusema kwamba tamaa za dunia hazitoki kwa Bwana. Tukitambua hili, kwa nini tunaendelea kuzitafuta? Kwa nini tunaendelea kuzipa kipau mbele kuliko vile vinavyompendeza Bwana?

Kuanza kuachana na ufujaji wa maisha, lazima tumuombe Mungu atusaidie kuacha kufuja maisha. Tunamuhitaji atufunulie mambo ya Mungu na mambo mazuri tuu, kwa sababu kuna mambo tunayaona kama mazuri, ambayo siyo lazima yawe ni dhambi, lakini ni ufujaji, kwa sababu hayatimizi kusudi la Mungu katika maisha yetu.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/