YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 7 OF 30

Wanafunzi kwanza walishindwa kutambua baraka ya ndoa inayotakiwa kudumu mpaka kufa. Walitawaliwa na mawazo ya wakati ule kwamba mke akionekana analeta matatizo kwa mumewe, basi ni kumpa tu hati ya talaka na kumwacha. Yesu anakubali kwamba si wote waliojaliwa kulipokea neno hili, yaani kulielewa. Kukubali uaminifu hadi kufa kunatufanya tutafute namna ya kutatua matatizo yetu badala ya kuyakimbia tu! Pia anaeleza kwamba wako kweli watu ambao hawawezi kuoa ("matowashi") kutokana na hali yao ilivyo.