YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 19 OF 30

Kiongozi asiyefuata maagizo ya Mungu ni kipofu naye atawapoteza wote wanaomfuata. Waisraeli walipomfanya Yeroboamu kuwa mfalme, aliwafanya wamwasi Mungu kwa dhambi nyingi. Hata majirani, yaani watu wa Yuda, waliathirika.Watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe(m.19). Kwa hiyo BWANA alikataa Israeli (= ufalme wa kaskazini) kama taifa, akawatupa wote, wakatekwa na kuwa watumwa.Bwana akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake. ... hata Bwana akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo(m.20, 23). Tukitulia na kutafakari tutagundua kuwa tunayosoma hapa yanalingana sana na hali yetu siku hizi, mbele za Mungu. Somo linakusukuma kufanya nini?