YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 18 OF 30

Katika mwaka wa 12 wa utawala wa Ahazi huko Yuda, Hoshea alianza kutawala Samaria. Alifanya maovu mbele za Mungu. Waisraeli wakawa chini ya kongwa la mfalme wa Ashuru aliyewateka na kudai wampe kodi kila mwaka. Tunaonyeshwa kwamba dhambi dhidi ya Mungu ina madhara makubwa:Wakafuata ubatili, wakawa ubatili(m.15). Na Mungu alighadhabika sana, mpakahapana aliyesaliakati ya Waisraeli (m.18), kwa sababuhawakutaka kusikiaalipokuwa akiwaonya (m.14). Je, tunafanana nao?