YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 23 OF 30

Wajumbe wa Ashuru walionyesha jeuri kwa kutumia Kiyahudi ili Wayuda wasikie na kushawishiwa kujisalimisha. Walisisitiza kwamba kwa kumtegemea BWANA, Hezekia alikuwa anawadanganya watu, kwani hakuwepo mungu aliyewaokoa watu wake katika mikono ya mfalme wa Ashuru:Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake wakati wo wote na mkono wa mfalme wa Ashuru? Iko wapi miungu ya Hamathi, na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, na ya Hena, na ya Iva? Je! Imeuokoa Samaria na mkono wangu? Katika miungu ya nchi hizi zote, ni miungu gani iliyookoa nchi yao na mkono wangu, hata Bwana auokoe Yerusalemu na mkono wangu?(m.33-35). Jambo zuri alilofanya Hezekia ni kuwaonya watu wake wasijibu mashambulizi na kebehi walizosikia.Watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana amri ya mfalme ilikuwa kwamba, Msimjibu neno(m.36). Katika hali kama hiimtu aliye na ufahamu hunyamaza(Mit 11:12). Hezekia alimtukuza Mungu kwa kumwachia Yeye kujibu.