YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 20 OF 30

Mfalme wa Ashuru aliwaleta watu kutoka maeneo mbalimbali na kuwafanya waishi katika maeneo alimowatoa Waisraeli. Kwa sababu hawakumcha Mungu,Bwana akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao(m.25). Agizo la Mfalme kuhusu kujifunzakawaida ya Mungu wa nchi(m.27) huakisi wazo la kipagani kuwa kila eneo lina mungu wake na ni muhimu kujipatanisha naye. Pamoja na kukubali wazo la mfalme, watu waliendelea kuabudu miungu yao ya asili. Kuchanganya dini namna hii, hata leo ni chukizo kwa BWANA.