YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 16 OF 30

Daudi anaendelea kufunua hali yake inavyoonekana mbele ya wengine. Watu wengi, na hasa marafiki zake wanamwacha. Maadui zake wanatunga hila na fitina dhidi yake. Hata hivyo anavumilia lawama zote na fitina wanazofanya dhidi yake. Anajifanya kwamba hasikii wala hataki kuwajibu chochote. Anachofanya ni kutumia kinywa chake kumsifu Mungu badala ya kuwajibu maadui zake. Daudi anamua kuyaacha mambo yote mikononi mwa Mungu na kuamini kuwa shida na aibu yake itakwisha kwa sababu Mungu yu pamoja naye.