YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

DAY 18 OF 30

Majeshi ya muungano ya nchi tatu walipata nguvu baada ya BWANA kuwatimizia hitaji lao la maji na kuwahakikishia ushindi wa vita. Waliweza kuwapiga Wamoabu waliodanganyika kwa kuona vibaya maji ya mto, wakidhani ni damu.Si rahisi kufafanua matokeo ya tendo la kutisha la mfalme wa Moabu kumtoa mwana na mrithi wake kama kafara kwa miungu. Pengine maana yake ni kama tafsiri ya Biblia Habari Njema inavyosema kwamba Waisraeli walirudi nchini kwao kwa sababu walichukizwa mno na tendo hilo baya.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More