YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

DAY 21 OF 30

Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza(Zab 55:22). Ndivyo tushuhudiavyo katika somo la leo: Kuna mwanamke anayepata mtoto kwa muujiza. Baada ya miaka michache mwana huyu anakufa, lakini mama yake bado ni imara katika imani, na anaamua aende kumwona Elisha ili kumtwika Bwana tatizo lake. Mama huyu hataki kupata msaada kwa mwingine ila kwa Mungu tu, na tunasoma jinsi imani yake inavyopata thawabu, Elisha anapomrudishia mwanawe akiwa hai. Mungu anajibu maombi yetu, tumtegemee!

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More