YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 27 OF 28

Obadia aliishi wakati maadui walipoteka Yerusalemu na kuchukua mali zake. Ana ujumbe juu ya Edomu, kizazi cha Esau.Mungu anakasirikia Edomu na kuahidi kulipiza kisasi, maana walifurahia na hata kushiriki katika kupigwa kwa Yuda. Anaambiwa, Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele. Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao (m.10-11). Angalia kwa nini Edomu walifanya udhalimu huu juu ya taifa la kindugu, Walidanganywa na kiburi chao (m.3, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya)! Tukikosa huruma na unyenyekevu, na pengine kushangilia mateso ya wengine, Mungu atatuhukumu. Tujichunguze kuhusu unyenyekevu. Tumwombe Mungu atuumbie huo.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More