YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 24 OF 28

Mungu alikuwa amechagua Yerusalemu, mji aliouchagua Bwana miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke jina lake huko (m.21), na aabudiwe humo. Lakini matokeo yakawa tofauti kabisa. Watu wa Yuda wakaacha kumwabudu Mungu na wakaiabudu miungu na kufanya machukizo ya kila namna kuliko yote waliyoyafanya baba zao (m.22-24). Matokeo yake, Mungu aliruhusu washambuliwe na Shishaki, mfalme wa Misri, lakini hakuna habari ya mfalme kuacha dhambi zake. Sisi ndio kanisa ambalo Mungu anajivunia, tunapomwasi Mungu tukageukia njia zinazomchukiza, tunamfanya Mungu awe na ghadhabu na sisi.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More