YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 26 OF 28

Kumbe, hata kama kizazi chetu tumemkosea Mungu, yeye anaweza kubadilisha mambo, tukapata kizazi kipya chenye kumpenda na kumwabudu Mungu. Ndivyo ilivyotokea Yuda, hata bila Abiya kutubu na kumwombea mtoto wake. Asa anaamua kufuata kama alivyofanya babaye Daudi. Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake (11-13). Matokeo yake, anapata kibali kwa Mungu, uongozi wake unabarikiwa, na jamii inafurahia matunda ya uongozi bora. Tutumie nafasi tuliyo nayo kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa uaminifu, naye atabariki na kuyafanikisha maisha yetu.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More