YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 1 OF 28

Pauloni mtumwa wa Kristo Yesu (m.1), yaani amejiweka chini ya mapenzi ya Yesu Kristo kwa kila jambo la maisha yake! Je, wewe umefanya hivyo? Hii ni barua ya msingi kutoka kwa mtume Paulo. Humo amepanga kwa utaratibu mafundisho ya msingi juu ya imani ya Kikristo. Ina sehemu kuu mbili: 1. Imani ya Mkristo (1:18-11:36). 2. Matendo ya Mkristo (12:1-15:33). Paulo anahubiri Injili ya Mungu (m.1), ambayo ni habari njema inayomhusu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kristo ametajwa mara 7 katika somo la leo!

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More