YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 2 OF 28

Katika m.16-17 Paulo anaonyesha kuwa msukumo wake wa kutaka sana kuwatembelea Wakristo wa Rumi ni Injili yenyewe. Anaeleza mwenyewe sababu, Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. Kuijua Injili, yaani habari njema ya Yesu Kristo ni utajiri mkubwa kupita kiwango! Maana Injili ina uwezo wa kufanya jambo la ajabu ambalo hakuna kitu kingine duniani kinachoweza kulifanya, yaani kumwokoa mwanadamu! Haki ya Mungu inadhihirishwa ndani ya Injili, toka imani hata imani (m.17). Yaani kwa kuamini matendo ya wokovu ya Yesu Kristo mtu huhesabiwa kuwa mwenye haki mbele ya Mungu!

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More