YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

DAY 8 OF 28

Kabla hajawa Mkristo Paulo alielimika sana katika dini ya Kiyahudi. Alijua maswali ya udadisi ambayo Wayahudi wangeweza kumwuliza kutokana na mafundisho yake. Kwa hiyo ameamua mwenyewe kuyauliza maswali haya na kuyajibu moja moja. Hivyo anawafundisha Wakristo wa Rumi mambo ya msingi ya imani. Paulo anamlinganisha Myahudi na Mmataifa (m.1-2). Sisi tungeweza kumlinganisha Mkristo na Mmataifa na kujibu kama Paulo katika m.2 anaposema, Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Na Myahudi (au Mkristo) kuasi hakumfanyi Mungu kuwa mwongo. Paulo anasema, Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu (m.3-4)!

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More