YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 14 OF 30

Wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.Hapa tunaona jambo moja lililorahisisha kazi ya kueneza Injili wakati ule. Jambo hili ni kwamba katika kila mji walipofika katika safari zao za misioni neno la Mungu lilifahamika tayari. Maana katika kila mji palikuwapo kundi la Wayahudi waliokuwa na sinagogi waliposoma na kujifunza neno la Mungu. Kwa njia hiyo hata baadhi ya Wayunani walikuwa wamelisikia neno la Mungu na kumwamini Mungu wa Wayahudi. Ni hao waitwao "Wayunani waliomcha Mungu"(m.4, 17).

Scripture