YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 17 OF 30

Kwa idadi ya watu, Korintho ulikuwa mji mkubwa kama Athene. Mungu alikuwa na mpango maalumu kwa Paulo hapo. Kwanzaaliwaendea Wayahudi kama kawaida yake. Kwa nini? Kwa sababu Injili ... ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia(Rum 1:16). Lakini ingawa aliwahubiria kwa bidii walipinga kwa nguvu (m.5-6: Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa). Ndipoakawageukia Mataifa na wengi wao walimpokea Kristo (m.8: Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa). Na Bwana mwenyewe alimtia Paulo moyo:Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu(m.9-10). Na kweli, Paulo akakaa huko muda mrefu kuliko miji mingine aliyotembelea (m.11:Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu). Kuhusu maisha yake Paulo alijitegemea. Zingatia m.3,Akakaa kwao[Akila na Prisila], wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema. Na 20:34, Mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.

Scripture