YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 22 OF 31

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu (m.33). Yesu amewaeleza wazi yale yatakayotokea kwake (m.28-30). Kwa hiyo yatakapotokea, wataamini ya kuwa yeye ndiye. Wataona ushindi wake na watakuwa na amani ndani yake. Yesu ni Bwana wa amani(2 The 3:16)! Ukimpokea yeye moyoni mwako utapata amani ya kweli! Amani nawaacheni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga(Yn 14:27). Dhambi zako zimefutwa kwa damu yake!

Scripture