Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Jamii ya watu haipendi kuishi katikati ya hali ya uovu. Kwa hiyo watu hupenda kuongozwa na kiongozi atendaye na kupenda haki na wema. Lakini dunia inashindwa kupata binadamu wanaoweza kutenda kwa haki na wema, ambazo ni tunu zitokazo kwa Mungu peke yake. Ndiyo maana haki na wema vitadhihirika wazi ajapo Kristo. Utawala wa Kristo unaleta heri kwa watu wote. Hata kama taifa na watu watapata shida katika maisha yao, iko siku ambayo Mwana wa Mungu atatawala kwa haki kinyume na watawala wa dunia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

