Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Watu wote wanaalikwa wamsikilize Mungu. Mungu ameghadhibika dhidi yao. Uumbaji wote mbinguni na duniani umeguswa na hasira hii. Ghadhabu ya Mungu inatokana na hali ya uovu. Maovu si mapenzi ya Mungu. Mataifa na watu wote wanaompinga Mungu na shuhuda zake, wajue kuwa mwisho wao upo.Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya(Isa 34:16). Kufanyike nini ili wapate kupona? Ni kuwa na bidii katika kusoma Neno la Mungu. Yesu Kristo ndiye anayetuepusha na hasira ya Mungu, kwa sababu yeye amebeba dhambi zetu msalabani. Yohana Mbatizajiamwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! (Yn 1:29).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

