Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 23 YA 30

Kuanzia sura hii ujumbe wa nabii umebadilika. Badala ya laana na hukumu na faraja kiasi kwa waliosalia na utunzaji wa Mungu kwao, sasa kuna tangazo jipya linalohusu uzuri na kutiwa moyo. Huruma na haki ya Mungu vinatangazwa hadharani. Rudia kutafakari m.3-6: Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea.Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Watu walio dhaifu na wanyonge wanapewa nguvu. Mungu amesimama upande wao. Huruma ya Mungu inawajia wote ambao licha ya udhaifu uliosababishwa na dhambi, wanahakikishiwa juu ya uwepo wa upendo wa Mungu kwao. Wajibu wao sasa ni kumtegemea huyu Mwokozi.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz